KONGAMANO LA WIKI YA UTALII "KARIBU KUSINI"

MUCE walichaguliwa kuwa wenyeji wa kongamano lililofanyika tarehe 13 Disemba 2018 kwenye ukumbi wa mihadhara.

Mada zilizowasilishwa ni:

1. Umuhimu na mchango wa utunzaji wa mazingira katika kukuza utalii nchini;

2. Umuhimu wa michango wa miundombinu katika kukuza utalii nchini; na

3. Namna mipango ya matumizi bora ya ardhi inavyochochea ukuaji na uhifadhi wa vivutio vya utalii nchini.